Saturday, July 21, 2012

14 wauawa katika shambulizi Marekani


 20 Julai, 2012 - Saa 14:08 GMT
Ukumbi wa Sinema mjini Denver
Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini Denver huko Colorado.
Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu. Alisema kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.
Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa kama ninja aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu kumi na wanne na kuwajeruhi wengine takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.
Walioshuhudia tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenye ukumbi huo mtu huyo akaanza kuwafyatulia watu waliokuwemo risasi.
Polisi wanasema kuwa walimtia mbaroni mtu mmoja katika eneo la kuegesha magari karibu na eneo la tukio.Akiwa na bunduki mbili. Wanaamini huenda silaha nyingi ziliachwa ndani ya ukumbi.  Mshukiwa huyo alisema kuwa aliacha mabomu katika nyumba yake kwenye jumba moja.Watu wameamrishwa kuondoka kwa jumba hilo.

SOURCE: bbcswahili.com

No comments: