Saturday, July 21, 2012

Hatarii - Nani kasema Mapadri hawatoi Rushwa? Soma hii


Padre mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police... 
Police akiwa anahitaji "Rushwa" alianza kuhoji.. 
 POLISI: Mbona gari yako inatoa Moshi mwingi?  Gari Matairi
       yameisha?


Hatimaye Polisi akamuamuru Padre waongozane kuelekea kituoni. Wakiwa njiani Polisi alimuuliza Padre...

POLISI: Umesema wewe ni Padre?
PADRE: Ndio.
POLISI:Je una biblia ndani ya gari?
PADREndio ninayo...
POLISI: Egesha gari yako pembeni...Kisha nipatie hiyo Biblia...

Padre akaegesha gari na kumpa biblia yule polisi...Polisi akasita kupokea kwanza, akamwambia Padre 

POLISI: Fungua na usome Mathayo 5:25-26

"Mtu wa Mungu akaanza kusoma....."

"Malizaneni na aliyekukamata kukupeleka mahakamani....Malizaneni upesi.. yamalize mambo haya mngali bado njiani kabla hajakukabidhi kwa hakimu... ambaye aweza kukuhukumu na kukukabidhi kwa bwana jela ili akutie gerezani. Amin nakwambia hautaachiwa hadi umetoa senti ya mwisho... 

Mtu wa Mungu alikubali kutoa yaliyo ya kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'Msiifanye migumu mioyo yenu.. nenda na Amani!
 

No comments: