Tuesday, July 24, 2012

NEWS ALERT: MABASI YA DAR EXPRESS NA SIMBA MTOTO YAGONGANA USO KWA USO LEO MAENEO YA WAMI



Abiria wakishushwa kupitia madirishani baada ya  Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na Basi la Simba mtoto lililokuwa linaenda Tanga kugongana uso kwa uso maeneo ya Wami kiasi cha masaa mawili hivi yaliyopita. Mwanahabari wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa yaliyoropotiwa ila watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.
 Uso kwa uso
 Abiria wakijaribu bila mafanikio kumuokoa mwenzao aliyenaswa
 Mmoja wa majeruhi
 Mama akiwa anaugulia pembeni mwa barabara
Abiria wakiendelea na juhudi za kuwatoa wenzao kutoka katika mabasi hayo

No comments: