Isabelle Ameganvi anasema kususia ngono kutasaidia wanawake kusikika |
Wanawake nchini Togo, wametakiwa kususia kitendo cha ndoa kuanzia
Jumatatu wiki hii kama njia ya kushinikiza serikali kuleta mageuzi. Kampeini hiyo yenye kauli mbiu ''Juhudi za
kuokoa Togo'' imeanzishwa kwa ushirikiano na mashirika tisa ya kijamii pamoja na
vyama saba vya upinzani pamoja na vyama vingine vya kijamii.
Kiongozi wa upinzani,
Isabelle Ameganvi alisema kuwa kususia ngono huenda ndio itakuwa silaha
inayofaa kuweza kuleta mageuzi ya kisiasa. Muungano wa vyama hivyo pamoja na
mashirika yasiyo ya kijamii unataka Rais Faure Gnassingbe, ambaye familia yake
imeshikilia madaraka kwa miaka mingi waweze kuondoka mamlakani.
"tuna njia nyingi
za kuwashinikiza wanaume kuelewa tunachotaka sisi wanawake'' alisema bi
Ameganvi, kiongozi wa tawi la wanawake la muungano huo.
Vurugu Togo |
Togo imekuwa
ikiongozwa na familia moja kwa zaidi ya miaka arobaini. Rais Faure Gnassingbe
alichukua mamlaka mnamo mwaka 2005 kufuatia kifo cha babake Gnassingbe Eyadema,
aliyetawala Togo kwa miaka 38. Rais alichaguliwa kwa muhula mwingine mnamo
mwaka 2010.
Alisema kuwa yeye ameweza kushawishiwa na mgomo sawa na huo nchini Liberia mwaka 2003, ambao walitumia njia ya kususia ngono kushinikiza amani. "ikiwa wanaume watakataa kusikia kilio chetu, tutalazimika kufanya maandamano ambayo yatakuwa makali zaidi kuliko mbinu hii ya kususia ngono.'' aliongeza bi Ameganyi.
Mgomo huo ulitangazwa
katika mkutano wa hadhara mnamo siku ya Jumamosi mjini Lome, na ambao
ulihudhuriwa na maelfu ya watu. Mkutano huo ulifanyika
kupinga mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa ambayo wakereketwa wanasema
kuwa yatarahisisha ushindi wa chama tawala cha Gnassingbe kuweza kwenye
uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwezi Oktoba.
Wanaharakati wanasema
kuwa mgomo huo utashinikiza wanaume ambao hawajihusishi na mchakato wa kisiasa
kuweza kuhakikisha malengo yake yanatimizwa ambayo ni pamoja na kukomeshwa kwa
utawala wa Rais usio na kikomo. Mapema mwezi huu, waandamanaji wanaopinga
utawala wa Rais Gnassingbe walitawanywa na polisi kwa kutumia gesi ya kutoa
machozi na wengine zaidi ya mia moja wakakamatwa.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment