Asilimia 35 ya wabunge wameng`oka majimboni
Email
Print
Comments
Wakati takribani asilimia 35 ya wabunge wote wa majimbo wameshindwa kutetea nafasi zao katika kura za maoni za vyama vya CCM, CUF na Chadema, mikoa ya Iringa, Tanga, Morogoro na Mwanza imetia fora kwa kuwatosa wabunge sita kila mmoja.
Wabunge hao sita kila mkoa ni wake waliokuwa wanasaka nafasi hiyo tena kupitia CCM.
Idadi ya wabunge waliopoteza matumaini ya kutetea nafasi zao kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia majimbo ni takribani asilimia 35 wa wabunge wote 232 wa majimbo.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa hadi kufikia jana, waliokuwa wabunge 68 kupitia CCM, mmoja wa Chadema na 12 wa CUF, walishindwa katika kura za maoni.
Idadi hiyo inafanya jumla wa waliokuwa wabunge hao kupitia majimboni kufikia 81 kati ya 232 waliokuwa bungeni na wanaotokana na majimbo.
Mikoa iliyotia fora
Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini), Profesa Raphael Mwalyosi (Ludewa), Jackson Makwetta (Njombe Kaskazini), Monica Mbega (Iringa Mjini), Yono Kevela (Njombe Magharibi) na Benito Malangalila (Mufindi Kusini).
Mkoa wa Tanga ni Joel Bendera (Korogwe Mjini), Balozi Abdul Mshangama (Lushoto), William Shelukindo (Bumbuli), Laus Mhina (Korogwe Vijijini), Bakari Mwapachu (Tanga Mjini) na Abdallah Rished (Pangani).
Mkoani Morogoro ni Hamza Mwenegoha (Morogoro Kusini), Castor Ligalama (Kilombero), Dk. Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi), Suleiman Sadiq Murad (Mvomero), Clemence Lyamba (Mikumi) na Omar Mzeru (Morogoro Mjini).
Mkoani ni Mwanza waliotemwa ni Samuel Chitalilo (Buchosa), James Musalika (Nyang'hwale), Ernest Mabina (Geita), Jacob Shibiliti (Misungwi), Bujiku Sakila (Kwimba) na Raphael Chegeni (Busega).
Mikoa ya Kagera na Tabora inafuatia kila mmoja ukiwatosa wabunge watano wa zamani.
Mkoa wa Kagera waliokuwa wabunge na majimbo yao kwenye mabano ni Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini), Diodorus Kamala (Nkenge), Wilson Masilingi (Muleba Kusini), Freethan Banyikwa (Ngara) na Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini).
Tabora wabunge walioathirika kutokana na uamuzi wa wanaCCM na majimbo yao kwenye mabano ni Tatu Ntimizi (Igalula), Said Nkumba (Sikonge), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini), James Nsekela (Tabora Kaskazini) na Lucas Selelii (Nzega).
Mikoa ya Mara, Dodoma na Pwani na Mtwara ina wabunge wanne kila moja, waliokataliwa na wanachama wenzao wa CCM.
Kwa Mkoa wa Mara ni Profesa Philemon Sarungi (Rorya), Dk. James Wanyancha (Serengeti), Charles Kajege (Mwibara) na Charles Mwera wa Tarime aliyetokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mkoani Dodoma walioenguliwa ni pamoja na jabali la siasa, John Malecela (Mtera), Pascal Degera (Kondoa Kusini), George Lubeleje (Mpwapwa) na Ephraim Madeje (Dodoma Mjini).
Pwani ni Zainab Gama (Kibaha Mjini), Profesa Idriss Mtulia (Kibiti), Ramadhan Maneno (Chalinze) na Dk. Ibrahim Msabaha (Kibaha Vijijini).
Mkoa wa Mtwara ni Mohamed Sinani (Mtwara Vijijini), Raynald Mrope (Masasi), Suleiman Kumchaya (Lulindi) na Dunstan Mkapa (Nanyumbu).
Mkoa wa Kigoma unafuatia kwa kutowarejesha wabunge watatu.
Wabunge hao ni Kilontsi Mporogomyi (Kasulu Magharibi), Manju Msambya (Kigoma Kusini) na Felix Kijiko (Muhambwe).
Shinyanga, Arusha, Singida, Rukwa, Mbeya na Manyara imetosa wabunge wawili kila mmoja.
Shinyanga ni John Shibuda (Maswa) na Charles Mlingwa (Shinyanga Mjini).
Rukwa ni Ponsian Nyami (Nkasi) na Ludovick Mwananzila (Kalambo).
Arusha ni Felix Mrema (Arusha Mjini) na Elisa Mollel (Arumeru Magharibi).
Mbeya walioshindwa ni Esterina Kilasi (Mbarali) na Guido Sigonda (Songwe)
Kwa upande wa mkoani Singida, wabunge waliokumbwa na `upepo wa kukataliwa’ ni Mgana Msindai (Iramba Mashariki) na Juma Kilimbah (Iramba Mashariki).
Manyara ni Damas Paschal Nakei ( Babati Vijijni) na Omar Kwaangw' (Babati Mjini).
Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Kilimanjaro imeacha mbunge mmoja mmoja ambao ni Mudhihir Mudhihir (Mchinga), Msomi (Kigamboni) na Aloyce Kimaro (Vunjo).
No comments:
Post a Comment