Sunday, August 8, 2010

HII YA ZITTO IMEKAAJE?

7th August 2010
Chapa
Maoni
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema iwapo atarudi bungeni, atashughulikia, pamoja na mambo mengine, kuondolewa wabunge katika bodi za mashirika ya umma.
Zitto amesema hali iliyopo sasa inashangaza kuona baadhi ya wabunge wako kwenye bodi zaidi ya tano.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa ukaguzi ulioandaliwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alisema wabunge kuwepo kwenye bodi za mashirika ya umma kunasababisha mgongano wa kimaslahi hivyo kazi haziendi ipasavyo.
Alisema kwa sasa wabunge wameondolewa kwenye baadhi ya mashirika, lakini wengine bado wapo hivyo miongoni mwa wajibu wake itakuwa ni kupigania ili wabunge wote waondolewe katika bodi hizo.

No comments: