"Nani muislamu hapa?,"
Watu kimya. Karudia tena kimya
"Nani muislam hapa?".
Ghafla kamnyakuwa jamaa alikuwa karibu na mlangoni akaondoka nae! Kufika nje akamwambia,
"Samahani mkuu wangu najua nimekusumbua, naomba unisaidie kuchinja mbuzi"
Jamaa akachinja yule mbuzi, alipomaliza akasema yeye hawezi kumchuna mbuzi.
Jamaa akiwa na panga lenye damu akarudi tena msikitini!
Jamaa akiwa na panga lenye damu akarudi tena msikitini!
"Jamani nauliza humu nani muislamu?"
Jamaa wakamnyooshea kidole imamu wa siku ile. Imam akaanza kujitetea!
" Aah jamani mi kuswalisha siku 2 tu ndo nimekuwa muislamu sana?,hapana mimi si muislam ila nilikuwa najifunza mila za dini hii tu."
Jamaa akasema
"naomba uondoe hofu naomba ukanisaidie kuchuna mbuzi nje!"
1 comment:
dUH! WANA IMANI HABA KWELI, WAKAJUA HAPO KUNA KITU CHA KUHALALISHWA.
Post a Comment