Monday, July 23, 2012

Kufuatia Ajali ya MV Skagit: Waziri wa serikali Zanzibar ajiuzulu




 

Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Hamad Masoud (Anayeonekana pichani kulia) amejiuzulu wadhifa wake baada ya kuwepo kwa shinikizo la kuachia ngazi lilitoka kwa wananchi.

Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka visiwani Zanzibar bila yeye kuchukua hatua. Amesema amejiuzulu kuonyesha uwajibikaji kisiasa lakini sio kwamba kiufundi yeye anawajibika kwa ajali hiyo.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kupitia blog hii

No comments: