Monday, July 23, 2012

Usalama wa Hotel Uko wapi? Wale mnaosafiri tusaidiane

Unaenda hotel unaambiwa ina usalama wa kutosha. Nje mwonekano wake ni wa kuvutia, uzio mnene, na security guard akiwa getini. Kwa upande wangu huwa napenda kujua hali halisi ya usalama wa hotel niifikiayo kila ninapokuwa safarini. Lakini huwa nashangazwa ninapoingia chumbani na kukuta tangazo mlangoni, au karatasi ya maelezo mezani kuwa, "ACHA/KABIDHI VITU VYAKO VYA THAMANI PALE RECEPTION VIKIWEMO HELA, SIMU, LAPTOP NK, HOTEL HAITAHUSIKA NA UPOTEVU WOWOTE" Je usalama wa hoteli hiyo utaupimaje? Au kwa nje ni salama, ila kwa ndani hawako salama. 


Je? wahudumu ndio tatizo? 
au wahusika wa hotel wanataka kujua tunakuwa na vitu gani vya thamani? 

Maana hata nyaraka tunazokuwa nazo ni za thamani na pengine zaidi ya hela, laptop au simu. Je na hizo nyaraka tuzikabidhi kaunta? maana ni siri na hawatakiwi kuzijua, na mwizi hachagui cha kuiba, na nguo ya ndani je? tuache kaunta? maana nayo ni ya thamani. Jamani nisaidie kuchekecha hiki kitu kichwani ili wenye Mahotel watuambie usalama wa hotel zao uko wapi? Ni uzio mnene kwa nje au ni ndani ya vyumba?

No comments: