Friday, July 20, 2012

Matukio katika Picha ajali ya meli ya Skagit Zanzibar



Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti zinavyoendelea. 
Mama alietambulika kwa Jina la Bitatu Uyelo ambae amenusurika na Kupoteza Mtoto wake wa miezi tisa katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe ikitokea Dare es salaam. 
Baadhi ya Maiti Walioopolewa kutoka katika ajali ya Meli ya Skagit iliozama hapo juzi walitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuwachukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.   Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli  ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar. 

Makazi ya milele. Wananchi wakijiandaa kuhifadhi Mhanga wa ajali ya meli
Baadhi ya Maiti walioopolewa kutoka katika ajali ya Meli iliozama na kukosa watu wake walipokelewa na kuzikwa na Serikali katika Eneo lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio. 
Wananchi wahiwahifadhi Baadhi ya Maiti Walioopolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hiyo. 
Vyombo vya usalama vikishirikiana  na Wananchi kuwasitiri Baadhi ya Maiti waliookolewa kutoka katika ajali ya Meli iliozama na kukosa watu wake katika Eneo lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio. 


 Bilal awafariji Wafiwa na Wahanga wa ajali ya meli 
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alimtembelea Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufuatia Msiba huu wa Ajali ya meli


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja,  Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.

Rais Kikwete Afika Zanzibar Kufariji Waliopatwa na Maafa 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali  July 19, 2012. 


 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, wakipata maelezo kutoka kwa daktari wa jeshi la Polisi anaeshughulikia vinasaba (DNA), Dk. Ahmed Makata, alipofika katika eneo la kuhifadhia maiti wa ajali ya kuzama meli ya MV.Skagit, kwenye viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana. 
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja July 19, 2012 
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi  July 19, 2012. 





MAKAMU WA PILI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR BALOZI SEIF IDD NAYE ALISHIRIKI KATIKA HATUA MBALIMBALI KUFUATIA MSIBA HUU WA KITAIFA 



Hapa akipokea Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema juu ya uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi kutokana na ajali iliyotokea.
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd akiwapa pole baadhi ya Watalii waliopata ajali wakati wakisafiri kwenda Zanzibar. Kwenye picha kushoto ni Waziri Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad

Hapa Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Akifuatana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine wakiwapa pole waathirika wa ajali ya meli.

Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd akizungumza na Wabunge wa bunge la Tanzania waliofika ofisini kwake kutoa mkono wa pole

  • PICHA KWA HISANI YA  MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII 

No comments: