Tuesday, October 9, 2012

Makampuni ya china tishio kwa Marekani - Mambo yaanza kuwa magumu kwa Wamarekani

Kamati ya bunge la Congress la Marekani imeyataka makampuni mawili makubwa ya simu za Kichina, Huawei na ZTE, kupigwa marufuku katika soko la Marekani.
Rasimu ya ripoti ya kamati ya bunge hilo kuhusu usalama, imesema makampuni hayo hayataweza kuaminika kuwa hayana ushawishi wa serikali ya Uchina na hivyo kuhatarisha usalama wa Marekani na taasisi zake.
Hata hivyo makampuni hayo yamekanusha kuendeshwa kwa ushawishi wa serikali ya Uchina.
Mwezi uliopita, Rais Obama alizuia kampuni moja ya Kichina kununua mashamba ya kuzalisha kawi ya upepo, pia akielezea kuwepo wasiwasi wa usalama wa taifa.

No comments: