Monday, September 26, 2016

MATEMBEZI YETU HIFADHI YA TAIFA UDZUNGWA - TANZANIA


MITI INAVYOTAMBULIKA KITAALAMU
AMBAYO MIZIZI NA MAJANI YAKE INATUMIKA KWA TIBA
 
MITI INAVYOTAMBULIKA KITAALAMU MIZIZI NA MAJANI YAKE INATUMIKA KWA TIBA  YA TIBA YA ASILI



MITI INAVYOTAMBULIKA KITAALAMU
AMBAYO MIZIZI NA MAJANI YAKE INATUMIKA KWA TIBA 
MAPOROMOKO YA SANJE
(SANJE WATER FALLS)
MAPOROMOKO YA SANJE
(SANJE WATER FALLS)
UOTO WA ASILI UNAVYOPENDEZA



Tuesday, March 8, 2016

Eden garden, Where Adam & Eve Leaved

People who leave at the Eden garden, where Adam & Eve leaved. See how human and wild animal leave together. and the wild animal ie. Giraffe feeding freely aside a house.

Thursday, June 19, 2014

UPI NDIO KWELI KUHUSIANA NA HIZI DINI TULIZOLETEWA?


Binafsi napatwa na mashaka sana linapokuja suala la dini na mapokeo yake hasa hizi dini zilizokuja kwa meli kutoka kwa wenzetu. Nikiwa nimelelewa katika maadili ya dini ya Kikristo, na ingawa naamini hata maadili ya dini ya Kiislamu hayatofautiani sana na yale ya Kikristo, nitaomba ndugu zangu mnisaidie kama kweli mafundisho yaliyoko kwenye Biblia yanaendana na uhalisia ulivyo. Baadhi ni kama ifuatavyo:- 



  1. Eti zamani hakukuwa na dhambi, ila baadaye kiburi "kikaonekana" ndani ya Lucifer (Ibilisi) aliyetaka kujiinua ili awe sawa na Mungu. Ndipo Mungu akamtupa kuzimu yeye na theluthi moja ya malaika. Na haya yote yalitokea kule kule Mbinguni. SWALI: IWEJE BABA ALIYE MTAKATIFU AUMBE KIUMBE KILICHOKUJA KUWA NA HITILAFU KAMA LUSIFA? Je, tuna uhakika gani kama hata watakaourithi Ufalme wake kule kule mbinguni hataibuka tena Lusifa mwingine akaasi kama ilivyokuwa kwa shetani? Mungu Anathibitishaje pasipo kuacha chembe ya shaka kuwa udhaifu katika mbingu ya mwanzo hautajirudia tena huko mbeleni? Ni nini kilimfanya ashindwe kumdhibiti Lusifa hadi akaleta uharibifu wote huu, na je, tuna uhakika gani kama sasa uwezo wa kudhibiti maasi kama hayo huko mbeleni anao?
  2. Eti alimtuma Yesu aje awafie wanadamu ili waokolewe na dhambi zao! Kwani ni nani mwingine aliyekuwa akitoa msamaha tofauti na yeye Mungu? Kama ni Mungu, iweje yeye huyo huyo adai damu ya mwanae imwagike? Ili iweje kwanza, wakati yeye huyo huyo alikuwa na uwezo wa kusamehe tu bila hata ya kumtoa kafara mwanaye? Au hiyo damu ilikuwa kwa ajili ya matambiko?
  3. Eti Yesu alikufa ili KILA AAMINIYE aokolewe......wakati huo huo Yesu huyo huyo kwenye mafundisho anasema njia iendayo uzimani ni NYEMBAMBA na wapitao huko ni wachache! Yohana anaenda mbali zaidi kwa kusema eti anaijua hesabu ya watakaoingia mbinguni kuwa ni mia moja arobaini na nne elfu tu! Ina maana katika dunia ya watu karibia 10 bil. ni 144,000 tu ndio watakaookolewa. Yaani pamoja na mbwembwe zote za Yesu, mitume wake na manabii kampeni hii yote ni kuokoa watu kiduchu namna hii? Hivi kuna Baba anayeweza kuwa na mkakati kama huu kweli?
  4. Kama Mungu ana nia ya kuokoa, iweje njia ya kwenda kwake iwe complicated namna hii? Binadamu ambaye kamuumba yeye mwenyewe ka-prove failure kutunza Amri zake 10. Mpinzani wake ambaye hata hana wahubiri, kanisa wala msikiti na wala hahitaji kutoa ndio ana wafuasi kibao, yaani 9,000,000,000 - 144,000! Hii ni hadaa kwani hata kama wewe ni mzazi na ukaona mwanao amepotea, huwezi kuweka masharti ambayo ni kama hayawezekani kutimizwa ili umuokoe, unless God is not rational!
  5. Haya, baadhi ya mafundisho yanachekesha. Eti akupigaye kwenye shavu la kushoto mgeuzie akunyuke na la kulia, heri maskini maana hao ufalme wa Mungu ni wao, mara Yesu akawa anawaambia wayahudi kuwa kuna baadhi wasingekufa hadi hapo ufalme wa Mungu utakapokuja! Leo ni miaka zaidi ya millenia 2 hajaja na hao aliokuwa anawaambia wasingekufa majina yao yameshasahauliwa ktk historia ya dunia hii.
  6. Yesu anasema "NAJA UPESI", how upesi is upesi? Hadi leo sijui kakwama wapi. Wapo wenzangu na mie walioacha shughuli zao na kwenda porini kumngojea, wengine walikufa na wengine kughairi na kuona upuuzi na kurejea mzigoni!
  7. Eti heshimuni mamlaka zilizopo duniani, kwa maana hakuna mamlaka iliyopo duniani ambayo haikuwekwa na Mungu! Serious? Hata ya Hitler, Saadam, Idd Amin, Gaddafi, Assad, JK, Kibaki, Museveni, Castro, etc zote hizi Mungu ndio aliziweka? Kama ni kweli basi tuna kila sababu ya kuhoji nia ya Mungu kwa wanae. Ukienda Syria ukaona watu wanavyouawa na kuchinjwa kama kuku halafu ukawahubiria watu wa Syria kuwa muheshimuni Rais Assad maana kawekwa na Mungu sidhani kama utatoka mzima! Itahitaji kuwa na akili ya kiuendawazimu kutetea fundisho hili!

My Take: Huenda hizi zilikuwa ni stori tu za wazungu ili kutupumbaza na kutuingilia watutawale. Kule Uyahudini ambako inasadikia Yesu alizaliwa wananchi wa kule hawana habari hizo na wengine wanaamini hajaja na wanamsubiria aje. Lakini wenzangu na mimi tulioko K'Koo ndio tunakomaa as if sisi ni majirani wa lile hori alilozaliwa! Hata kule Mecca ambako Mtume aliishi na wake zake, Saudi Arabia leo wanajenga vyoo vya umma na hoteli. Lakini wenzangu na mie tulioko Kwamtoro tunakomaa kama vile Muhammad alizaliwa Magomeni Mapipa! Pia, wazungu wenyewe ambao ndio walituletea hizi imani sasa hawana time na mambo haya. Ulaya wanaosali/kuswali ni wazee na ni wachache sana. Vijana na watu wengine wengi wako busy kutafuta hela! Lakini sisi ambao hizi stori tuliletewa ndio tunataka hata siku za kufanya kazi zipungue ili watu wawe na muda wa kusali/kuswali! 
Sikusudii kukashifu imani za watu, ila lengo langu ni kutaka uelewa zaidi juu ya mapokeo haya maana tumeanza kushuhudia HASARA ya mapokeo haya ambayo watu wanayapokea pasipo kutumia akili ya kawaida kuhoji. Sasa hivi dini ndio inataka kuwa chanzo cha social unrest tofauti na enzi za mababu zetu ambao waliishi kwa amani na upendo licha ya kuwa wazungu waliziita dini zetu kuwa ni za kishezi! Sasa upi ni ushenzi, dini zilizokuwa zinaunganisha watu na kuwa wamoja bila kubaguana kwa vyovyote vile au hizi za kileo ambazo zime-prove failure katika kuleta amani na utulivu duniani? 

Only in Tanzania you can see these amazing nature.

Say something about this Hippo
What can you say about this crest?
Any word to this python or to the antelope?

Friday, May 30, 2014

Maelezo ya Zitto Zuberi Kabwe (Mb) juu tuhuma za kufisadi Fedha za NSSF na TANAPA zilizotolewa ndani ya bunge la Tanzania


Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.

Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF.

Mh. Zitto Kabwe
Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.

Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi zao mbalimbali.

Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande wa TANAPA wasanii hawa waliandaa kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadani na walilipwa. Kwa upande wa NSSF wasanii hao walitunga wimbo na video yake (http://m.youtube.com/watch?v=sMl8T-RkIdM ) na wimbo huo unatumika katika Shirika hilo. 
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.

Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.

Toka mwaka 2012 nilipoanza kujitokeza kusemea wasanii watu kadhaa wenye maslahi na tasnia hii wamekuwa wakinikatisha tamaa na hata wengine kuona nimewaingilia kazi zao. 
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.

Inaniumiza zaidi kutokana na ukweli kwamba ninamwuguza mama yangu mzazi, kipindi ninachohitaji kutiwa moyo na kuombewa hata na maadui zangu kisiasa. Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama ambacho watoa tuhuma wanatoka, pole ninayopewa ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

Najua wajibu wangu ni kusimamia Mashirika ya Umma na nikiwa mpigania uwajibikaji nipo makini sana kuhakikisha sina mgongano wa maslahi katika mambo yangu. Ndio maana sina biashara yeyote ile ili kuhakikisha natimiza wajibu wangu kwa uadilifu mkubwa. Napata 'moral authority' ya kutaka uwajibikaji kwa sababu nafanya kazi zangu kwa misingi hiyo 'at arms length'.
Hivyo ninataka mara moja CAG afanye ukaguzi wa kazi za wasanii hao kwenye NSSF na TANAPA. Pia achunguze kama Gombe Advisors ( company limited by guarantee) ina maslahi yeyote ya kifedha katika kazi hizo za wasanii. Nataka pia Shirika la NSSF na TANAPA waweke wazi mchakato wa kazi zao na wasanii hawa kupitia LEKADUTIGITE Limited.

Zitto Kabwe
Mei 29, 2014

Dar Es Salaam.

Thursday, January 3, 2013

SIJUI KUNA KIRUSI KIMEPITA HAPA MAONO YANGU...

Wadau kwa muda sasa nimekuwa kimya na mkawa hampati Visa na Habari motomoto sio kwa mapenzi yangu, Ila kuna kidudu mtu kaingia humu kwenye blog na amejaribu kucheza na mimi ki Digitali, Lakini nafikiri sasa atashangaa.

Tushirikiane tu. Nipo kwenye vita kali ya Digitali, ni Zaidi ya Vita Kuu ya Nne ya Dunia.

Wednesday, December 5, 2012

VIPIMO VYA DNA VYA MWAKA HUU VYAONYESHA KARIBU NUSU YA WATOTO AKINA BABA WAMESINGIZIWA KUWA NI WAO


ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.
Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.
Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.
Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote.
“Hatusemi kuwa sasa  wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo,” alisema.
KUSOMA ZAIDI HABARI HII NENDA: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wednesday, November 14, 2012

Sizitaki Mbichi hizi - Hii ni kwa wale wa zamani

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi

Thursday, October 18, 2012

Dk Ulimboka asema Mfanyakazi Ikulu alihusika kumteka

HATIMAYE Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka ameamua kuvunja ukimya, baada ya kumtaja kinara wa tukio la kutekwa kwake na kisha kutupwa kwenye Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa Julai 26, mwaka huu.

Dk. Ulimboka amemtaja mtu huyo katika taarifa yake iliyosomwa jana jijini Dar es Salaam na wakili wake, Nyoronyo Kicheere. Maelezo katika taarifa ya Dk Ulimboka, yanadaiwa kushuhudiwa na wakili mwingine wa kujitegemea, Rugemeleza Nshala.

Taarifa hiyo pia ilisema mtu aliyekuwa na Dk Ulimboka kabla ya kukamatwa kwake alitambulishwa kwao na kigogo ambaye hakumtaja jina, kwa makubaliano kuwa atakuwa anachukua madai ya madaktari dhidi ya Serikali.

“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa,” inaeleza taarifa hiyo na kuonyesha namba za simu za mtu huyo anayedaiwa ni mfanyakazi wa Ikulu.

“Ninamfahamu sana bwana (jina tunalihifadhi kwa sasa), kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile. Nakumbuka alitambulishwa kwetu na kigogo mmoja nikiwa pamoja na wawakilishi wengine wa madaktari,” alisema.

Katika taarifa hiyo iliyoainisha namba iliyokuwa inatumiwa na Dk Ulimboka kuwasiliana na mtu huyo, inaeleza pia kuwa mpaka sasa mtu huyo yupo hai na kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo huru ili kuhakikisha haki inatendeka.

Taarifa inaeleza pia kuwa kwa nyakati tofauti mtu huyo alikuwa akitumwa kwa Dk Ulimboka na mtu ambaye tamko hilo halikumtaja, lengo likiwa ni kuchukua nyaraka mbalimbali na vyeti vya kuthibitisha taaluma za masomo yake.

“Wale wote waliotuhumiwa na ninaowatuhumu kunitendea unyama huu wako huru na hakuna aliyeguswa. Je uhai na maisha yangu, yana thamani ndogo kama ya mnyama anayekwenda machinjioni? alihoji Dk Ulimboka katika taarifa hiyo na kuendelea:

"Je Serikali ya nchi yangu itakubali lini kuundwa kwa tume huru kuchunguza unyama huu na kuhakikisha kuwa haki inatendeka?”

Dk. Ulimboka amesema katika taarifa hiyo kuwa: “Niko tayari kuhojiwa na kutoa ushirikiano wangu kwa vyombo huru na makini vya uchunguzi ambavyo vitaundwa ili kuweza kuubaini ukweli.”

Maelezo ya wakili wake
Akisoma taarifa hiyo jana, Kicheere alisema kwa sasa Dk Ulimboka yupo nje ya nchi kwa matibabu zaidi na aliandika tamko hilo mbele ya Wakili Nshala, ambaye pia ameweka saini na mhuri wake.

Hata hivyo, tamko hilo ambalo Kicheere alilisoma mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, linaonyesha lilitolewa Oktoba 7, mwaka 2011, jambo ambalo Nshala akizungumza na gazeti hili alisema ni makosa ya uchapaji.

“Hilo tamko lilisomwa mbele yangu Oktoba 7, mwaka huu, hiyo ya kuandikwa mwaka 2011 ni makosa ya uchapaji tu.” alisema Nshala.

Naye Kicheere alisema, Dk Ulimboka yupo tayari kusema ukweli wote wa kilichomkuta endapo itaundwa tume huru ya kuchunguza tukio hilo.

Alisema taarifa ambazo alizitoa na kurekodiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo mtandao ya kijamii, ni za kweli na alizotoa akiwa na akili na kumbukumbu nzuri.

Tamko hilo linaeleza kwamba, moja ya uthibitisho kuwa taarifa hizo alizozitoa kabla ya kufika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (Moi), na zile alizozitoa akiwa hapo, ni kule kuweza kumwita na kumshawishi mtu aliyemsaidia kutoka Msitu wa Pande.

“Uthibitisho wa kumbukumbu nzuri niliyonayo, ni pale nilipokutana na Juma Mganza katika Msitu wa Mabwepande asubuhi ya siku ya tukio. Pamoja na maumivu makali niliokuwa nayo kutoka kila sehemu ya mwili wangu, niliweza kumshawishi Mganza kunifungua kamba za mikono nilizokuwa nimefungwa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza;

“Pia kukumbuka namba ya simu ya rafiki yangu Dk Deogratias ambapo Mganza aliweza kuitumia kuwasiliana naye kumpa taarifa kuhusu tukio hilo. Ni kupitia taarifa hiyo ndipo suala la mimi kufikishwa Moi lilipofikiwa.”

Aliendelea: “Na kama niliweza kukumbuka namba ya rafiki yangu, mambo hayo yanatosha kuthibitisha kuwa ninachokisema ni ukweli na kuwa utimamu na kumbukumbu zangu ni sahihi”.

Usiku wa Julai 26, mwaka huu, Dk Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana na kupigwa vibaya ambapo Julai 27, alikutwa kwenye Msitu wa Pande uliopo Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Baada ya tukio hilo, alisafirishwa mpaka Moi ambapo baadaye alipelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

Sunday, October 14, 2012

IGP Mwema atoa taarifa rasmi kuhusu mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow.


Aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza
ACP Liberatus Barlow
Usiku wa kuamkia Tarehe 13/ 10/ 2012 zimepatikana taarifa zilizothibitishwa juu ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow. IGP Said Mwema ametoa taarifa juu ya mauaji hayo. 

Ifuatayo ni taarifa kamili kutoka kwa IGP Mwema: 
  1. Ndugu wananchi. Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kuhusu mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa polisi Liberatus Barlow yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia leo 13/10/2012 majira ya saa saba usiku Mkoani Mwanza.
  2. Tukio hilo limetokea wakati kamanda huyo akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Florida hotel Mwanza mjini, akiwa na ndugu yake waliyeongozana naye kutoka kwenye kikao hicho. Wakati akimshusha huyo ndugu yake eneo la Kitangiri minazi mitatu, walitokea watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, na kumvamia na kuanza kumshambulia kwa risasi na kumuua hapo hapo.
  3. Ndugu wananchi, kufuatia tukio hilo, tayari nimemtuma Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai DCI Robert Manumba kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha ulinzi na upelelezi wa tukio hilo. 
  4. Najua tukio hili limeshitua na kutuhuzunisha wote. Hivyo, wakati tukiendelea na taratibu zingine kuhusiana na tukio hilo, niwaombe wananchi wote kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao.
  5. Tutaendelea kuwapa taarifa za tukio hilo, kadri tutakavyoendelea kuzipata."

Thursday, October 11, 2012

China yahusishwa kuchochea ujangili wa tembo katika hifadhi za Tanzania

Bendera ya China
BAADHI ya mataifa ya Mashariki ya mbali ikiwamo China yamedaiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa vitendo vya ujangili katika mbuga za wanyama nchini kutokana na nchi hizo kuruhusu biashara ya pembe za ndovu. Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa mbali na China mataifa mengine ni  yanayochochea biashara  ya pembe ni Hong Kong, Japan na Korea Kusini. Mbali na kuwapo kwa hali hiyo, Serikali imesema pi inafahamu mtandao wa kimataifa unaolizalisha silaha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kijangili kwenye mbuga za wanyama nchini Tanzania.

Nyalandu alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuzungumzia pamoja na mambo mengine, kongamano la utalii linalotarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Arusha.
Ukuta mkuu wa China
mojawapo ya vivutio vikubwa vya utalii vya China
"Sisi tumefanya mapitio tukabaini vyanzo vya tatizo hili…tumegundua wateja wengi wa meno ya tembo wanatoka China. Kila msichana nchini China anavaa cheni iliyotengenezwa kwa meno ya tembo na matokeo yake, imepandisha gharama ya kilo moja ya meno hayo kutoka Dola 100  hadi Dola 1,000, hivi vyote ni vichochezi," alisema na kuongeza: "Hebu fikiria, China yenyewe ina watu zaidi ya bilioni 1, sasa jumlisha na wateja wengine kutoka Japan, Korea Kusini, Hong Kong na nchi zingine za Mashariki ya mbali."

Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Nyalandu alisema Serikali imeuomba upya Umoja wa Mataifa kuuza akiba yake ya meno ya tembo yaliyotaifishwa ili kupata fedha za kuimarisha ulinzi kwa lengo la kumaliza tatizo hilo la ujangili.

"Tukifanikiwa azma hiyo tutahitaji kupata ushirikiano wa karibu toka Jumuiya za Kimataifa wakiwamo polisi wa kimataifa ‘interpol’ na nchi wahisani ili kukamata bidhaa zake yakiwamo meno ya tembo yaliyosafirishwa kimagendo," alisema.

Mh. Lazaro Nyalandu
Naibu waziri wa wizara ya
maliasili na utalii
Nyalandu alisema kuwa vitendo vya ujangili vinaendelea kuwa tishio kwa mali asili ya taifa hivyo kunahitajika mkakati wa kukabiliana nao. Naibu Waziri Nyalandu alikiri ugumu uliopo wa kukabiliana na wimbi la vitendo vya kijangili ambao alisema unaziandama karibu nchi nyingi za Afrika, lakini alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuusambaratisha mtandao huo kwa vile wahusika wake tayari wanatambulika.

“Serikali inafahamu mitandao yote inayojihusisha na biashara haramu ya ujangili. Tunawafahamu wale wanatumika kuingiza silaha nchini na kufanya uhalifu. Lakini pia tunafahamu nchi duniani ambako meno haya ya tembo yanaenda na jinsi gani yanaenda na tumeiomba dunia tushirikiane katika hili,” alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema kuwa tatizo la ujangili wa meno ya tembo haliwezi kukabiliwa na nchi moja kwani limechukua sura ya kimataifa hivyo ni wajibu wa kila nchi kushirikiana na taifa lingine kufifisha hujuma zinazoendeshwa na mitandao hiyo. “Nenda Kenya hali ni ile ile, sasa sisi tunasema kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko tayari kukabiliana na ujangili huu na tunaomba wenzetu pia tushirikiane,” alisisitiza Nyalandu.

Naibu Waziri Nyalandu alisema kuwa mkutano wa kimataifa uliofanyika huko Doha chini ya mwamvuli wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii (UNTO) ulizima jaribio la Tanzania kuuza meno hayo ya tembo, lakini sasa Serikali inakusudia kutumia kikao kijacho kitakachofanyika Bangkok kupenyeza ushawishi wake ili iruhusiwe kuuza meno hayo.

Wakati huohuo Wizara ya Mali ya asili na Utalii itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 15 mwaka huu. Kongamano hilo ambalo litahusu usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi ya taifa na linatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 412 kutoka mataifa 40 ya Afrika.

SOURCE YA HABARI HII: http://www.mwananchi.co.tz

Uchumi wa Uingereza upo hatarini kuporomoka vibaya

David Cameron
Waziri Mkuu wa Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ameonya kuwa Uingereza itaanguka kiuchumi na kuvuta mkia nyuma ya Brazil, China na India iwapo haitapunguza nakisi ya bajeti yake na kuwa ya ushindani zaidi.
Bw Cameron ameuambia mkutano mkuu wa kila mwaka wa chama chake cha Conservative kuwa Uingereza inaweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuimarisha elimu yake, kupunguza matumizi katika ustawi wa jamii na kuausha ari miongoni mwa watu wake.
Ingawa imechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kwa Uingereza kurekebisha uchumi wake urejee kwenye kukua tena, Cameron amesema nakisi ya taifa imepunguzwa kwa kiasi cha robo katika miaka miwili iliyopita.