Wednesday, December 5, 2012

VIPIMO VYA DNA VYA MWAKA HUU VYAONYESHA KARIBU NUSU YA WATOTO AKINA BABA WAMESINGIZIWA KUWA NI WAO


ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.
Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.
Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.
Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote.
“Hatusemi kuwa sasa  wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo,” alisema.
KUSOMA ZAIDI HABARI HII NENDA: http://www.mwananchi.co.tz/habari

No comments: