Tuesday, September 25, 2012

Tutafakari haya....Misemo ya Kiswahili


  •  Waninunia mie.....umekosa mwenyewe magoli ya penati utayaweza ya kona.......
  • Japo chungu we meza tu....
  • Kufika utafika hata kama ukitembea....
  • Mola nipe jicho la tatu linijaze ufahamu....
  • Aliyekuonjesha kaweke kambi kwake.....
  • Eti kuku wa kuchora....hawiki, hatagi yai wala hadonoi.....
  • Unaacha nyama nyumbani unaenda kula mishikaki baa....
  • Umezoea cheko la nyundo hebu tupe la msumari sie nginjha nginjha....
  • Uko busy airport unasubiri meli na hata passport hujabeba.......
  • Umeumbwa u-kanga unataka u-kuku.....
  • Uko busy kama unapiga deki bahari.....
  • Japo chungu we meza tu......
  • Donda la maskini hupona kwa umande.....
  • Kobe hufika aendako hata akienda taratibu......
  • Usijifanye unachagua wakati bado unachaguliwa......
  • Hata tausi mrembo lakini haliwi nyama....
  • Mbwa mzee hafundishwi sheria mpya.....
  • Ingekuwa rahisi hata samaki angetafuta perfume......
  • Aaahhh papai kubwa ka-apple kadogoo...bei ya apple sasa, papai halina maana....
  • Uniniletea perege mie, hicho kidagaa....niletee yule papa ndio saizi yangu
  • Hukushiba kwa tonge, utashiba kwa kulamba....
  • Ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa......
  • Madogo madogo yakupite na makubwa yakusakame....
  • Huwezi kuwa mkwezi ukashindwa kusuka pakacha......
  • Mchele kisoda, nazi sita.....
  • Usipaki fuso kwenye gereji ya bajaji...
  • Usipite kimyakimya uliza njia usije ukajigonga buree...
  • Muwasho wa ulimi, haukunwi na kidole....
  • Kama bahari.....ukiweka lindo kaskazini wenzio kusini wanavua....
  • Mzoea punda, hapandi farasi.....
  • Bora kandambili kuliko mdundo mbovu....
  • Unavua samaki kwa mikono, utamaliza kesho.....
  • Ukibipu tu, mi nakupigia.....
  • Una maswali mengi, kwani we ni polisi.....
  • Unaniongelesha kizungu, umenisomesha wewe......
  • Mchuma janga, hula na wa kwao.....
  • Zege halilali.....
  • Ukimjua adui yako unamshinda kirahisi.....
  • Unapanda basi la bagamoyo wakati unaenda ikwiriri.......
  • Uko kama majani ya chai, hujulikani kama dawa ya ngiri au ya kichwa.......
  • Ameshakuwa kuku wa kwenye jokofu, kapoteza radha..........

No comments: