Thursday, June 19, 2014

UPI NDIO KWELI KUHUSIANA NA HIZI DINI TULIZOLETEWA?


Binafsi napatwa na mashaka sana linapokuja suala la dini na mapokeo yake hasa hizi dini zilizokuja kwa meli kutoka kwa wenzetu. Nikiwa nimelelewa katika maadili ya dini ya Kikristo, na ingawa naamini hata maadili ya dini ya Kiislamu hayatofautiani sana na yale ya Kikristo, nitaomba ndugu zangu mnisaidie kama kweli mafundisho yaliyoko kwenye Biblia yanaendana na uhalisia ulivyo. Baadhi ni kama ifuatavyo:- 



  1. Eti zamani hakukuwa na dhambi, ila baadaye kiburi "kikaonekana" ndani ya Lucifer (Ibilisi) aliyetaka kujiinua ili awe sawa na Mungu. Ndipo Mungu akamtupa kuzimu yeye na theluthi moja ya malaika. Na haya yote yalitokea kule kule Mbinguni. SWALI: IWEJE BABA ALIYE MTAKATIFU AUMBE KIUMBE KILICHOKUJA KUWA NA HITILAFU KAMA LUSIFA? Je, tuna uhakika gani kama hata watakaourithi Ufalme wake kule kule mbinguni hataibuka tena Lusifa mwingine akaasi kama ilivyokuwa kwa shetani? Mungu Anathibitishaje pasipo kuacha chembe ya shaka kuwa udhaifu katika mbingu ya mwanzo hautajirudia tena huko mbeleni? Ni nini kilimfanya ashindwe kumdhibiti Lusifa hadi akaleta uharibifu wote huu, na je, tuna uhakika gani kama sasa uwezo wa kudhibiti maasi kama hayo huko mbeleni anao?
  2. Eti alimtuma Yesu aje awafie wanadamu ili waokolewe na dhambi zao! Kwani ni nani mwingine aliyekuwa akitoa msamaha tofauti na yeye Mungu? Kama ni Mungu, iweje yeye huyo huyo adai damu ya mwanae imwagike? Ili iweje kwanza, wakati yeye huyo huyo alikuwa na uwezo wa kusamehe tu bila hata ya kumtoa kafara mwanaye? Au hiyo damu ilikuwa kwa ajili ya matambiko?
  3. Eti Yesu alikufa ili KILA AAMINIYE aokolewe......wakati huo huo Yesu huyo huyo kwenye mafundisho anasema njia iendayo uzimani ni NYEMBAMBA na wapitao huko ni wachache! Yohana anaenda mbali zaidi kwa kusema eti anaijua hesabu ya watakaoingia mbinguni kuwa ni mia moja arobaini na nne elfu tu! Ina maana katika dunia ya watu karibia 10 bil. ni 144,000 tu ndio watakaookolewa. Yaani pamoja na mbwembwe zote za Yesu, mitume wake na manabii kampeni hii yote ni kuokoa watu kiduchu namna hii? Hivi kuna Baba anayeweza kuwa na mkakati kama huu kweli?
  4. Kama Mungu ana nia ya kuokoa, iweje njia ya kwenda kwake iwe complicated namna hii? Binadamu ambaye kamuumba yeye mwenyewe ka-prove failure kutunza Amri zake 10. Mpinzani wake ambaye hata hana wahubiri, kanisa wala msikiti na wala hahitaji kutoa ndio ana wafuasi kibao, yaani 9,000,000,000 - 144,000! Hii ni hadaa kwani hata kama wewe ni mzazi na ukaona mwanao amepotea, huwezi kuweka masharti ambayo ni kama hayawezekani kutimizwa ili umuokoe, unless God is not rational!
  5. Haya, baadhi ya mafundisho yanachekesha. Eti akupigaye kwenye shavu la kushoto mgeuzie akunyuke na la kulia, heri maskini maana hao ufalme wa Mungu ni wao, mara Yesu akawa anawaambia wayahudi kuwa kuna baadhi wasingekufa hadi hapo ufalme wa Mungu utakapokuja! Leo ni miaka zaidi ya millenia 2 hajaja na hao aliokuwa anawaambia wasingekufa majina yao yameshasahauliwa ktk historia ya dunia hii.
  6. Yesu anasema "NAJA UPESI", how upesi is upesi? Hadi leo sijui kakwama wapi. Wapo wenzangu na mie walioacha shughuli zao na kwenda porini kumngojea, wengine walikufa na wengine kughairi na kuona upuuzi na kurejea mzigoni!
  7. Eti heshimuni mamlaka zilizopo duniani, kwa maana hakuna mamlaka iliyopo duniani ambayo haikuwekwa na Mungu! Serious? Hata ya Hitler, Saadam, Idd Amin, Gaddafi, Assad, JK, Kibaki, Museveni, Castro, etc zote hizi Mungu ndio aliziweka? Kama ni kweli basi tuna kila sababu ya kuhoji nia ya Mungu kwa wanae. Ukienda Syria ukaona watu wanavyouawa na kuchinjwa kama kuku halafu ukawahubiria watu wa Syria kuwa muheshimuni Rais Assad maana kawekwa na Mungu sidhani kama utatoka mzima! Itahitaji kuwa na akili ya kiuendawazimu kutetea fundisho hili!

My Take: Huenda hizi zilikuwa ni stori tu za wazungu ili kutupumbaza na kutuingilia watutawale. Kule Uyahudini ambako inasadikia Yesu alizaliwa wananchi wa kule hawana habari hizo na wengine wanaamini hajaja na wanamsubiria aje. Lakini wenzangu na mimi tulioko K'Koo ndio tunakomaa as if sisi ni majirani wa lile hori alilozaliwa! Hata kule Mecca ambako Mtume aliishi na wake zake, Saudi Arabia leo wanajenga vyoo vya umma na hoteli. Lakini wenzangu na mie tulioko Kwamtoro tunakomaa kama vile Muhammad alizaliwa Magomeni Mapipa! Pia, wazungu wenyewe ambao ndio walituletea hizi imani sasa hawana time na mambo haya. Ulaya wanaosali/kuswali ni wazee na ni wachache sana. Vijana na watu wengine wengi wako busy kutafuta hela! Lakini sisi ambao hizi stori tuliletewa ndio tunataka hata siku za kufanya kazi zipungue ili watu wawe na muda wa kusali/kuswali! 
Sikusudii kukashifu imani za watu, ila lengo langu ni kutaka uelewa zaidi juu ya mapokeo haya maana tumeanza kushuhudia HASARA ya mapokeo haya ambayo watu wanayapokea pasipo kutumia akili ya kawaida kuhoji. Sasa hivi dini ndio inataka kuwa chanzo cha social unrest tofauti na enzi za mababu zetu ambao waliishi kwa amani na upendo licha ya kuwa wazungu waliziita dini zetu kuwa ni za kishezi! Sasa upi ni ushenzi, dini zilizokuwa zinaunganisha watu na kuwa wamoja bila kubaguana kwa vyovyote vile au hizi za kileo ambazo zime-prove failure katika kuleta amani na utulivu duniani? 

2 comments:

Unknown said...

ASANTE NDUGU YANGU MKRISTO KWA ULIYOYASEMA. MIMI BINAFSI SIJAKERWA NA HAYO ILA KAMA KWELI HAYA ULIYOSEMA YANATOKA MOYONI, BASI NITAKUWA TAYARI KUTUMIA MUDA WANGU ILI TUCHAMBUE MCHELE NA PUMBA HADI TUFIKIE MAHALI PAZURI PA KUELEWEKA. NA NINAAMINI YOU ARE IN THE RIGHT TRUCK, KWA KUWA DINI MAANA YAKE SI KUMZUIA MTU ASIHOJI AU ASITUMIE AKILI.

Anonymous said...

Bw. Charles Ntogwisangu naomba kupata hayo mafundisho yako uliyonayo kutokana na hoja za mtoa mada.