Saturday, September 29, 2012

Je wajua sababu za Mwanaume kuwa na dalili za ujauzito yaani kizunguzungu, kutapika, kichefuchefu, tumbo kufura na kuwa na hasira kama mkewe mjamzito?

Ni kawaida kwa wanawake wengi wakati wa ujazito kuanza kutapika , kuwa ni kichefu chefu, kuhisi kisunzi au kizunguzungu, kujisikia wanyonge, hasa wakati wa asubuhi. Kiingereza inaitwa "Morning sickness"
Wataalam wanasema haina sababu moja. Lakini wanakubali kuwa husababishwa na ongezeko la homoni hasa ya Estrogen katika mwili wa mwanamke ambayo inaweza kumuongezea, uwezo wa kunusa harufu hasa mbaya. Pia Kuongezeka kwa maji aina ya gastroline.Je unafahamu kuwa mwanamume. Baba mwenye nyumba pia anaweza kuwa na dalili hizo hizo za ujauzito yaani?, kizunguzungu, kutapika , kichefu chefu , tumbo kufura na kuwa na hasira kama mkewe?
Kwa wakati huu Mike Dowdall, bwana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Manchester Uingereza amefura tumbo, anatapika tapika. Asubuhi hujisikia kisunzi au kizunguzungu na anapenda kula vitu vichachu kama maembe mabichi yaliyotiwa chumvi au pilipili. Mpenzi wake Amanda Bennett ni mjamzito. Dalili za Mike zilipoanza bi Amanda alichukulia kwamba mpenzi wake ambaye wameishi naye kwa miaka mitatu sasa anamfanyia mzaha au stihizai kwa kumuiga vile anavyotapika, na kupenda kula kula.
Lakini madaktari kutoka Manchster wanasema Bwana Mike ana ugonjwa wa mimba bandia. Wao wanaita "Couvade syndromehuu sio uchawi, bali ni ugonjwa unaoweza kuwapata wanaume. Tumbo kufura, kutapika tapika asubuhi, kuhisi kizunguzungu na kupenda kula maembe yaliyotiwa chumvi au pilipili.
Mike amekuwa na uja uzito bandia kwa wiki 33 na kama vile tu akina mama walio na mimba, ameongeza uzani kwa zaidi ya kilo 3 na sasa anajihisi mchovu kila mara, kuumwa na mgongo na kwenda haja ndogo kila mara. Madaktari hao wanasema ugonjwa huu unaweza kusababishwa na ile hali kuwa na wasiwasi unaposubiri mkeo kujifungua, au pia kuwa karibu sana na mkeo. Bi Amanda ambaye ana mimba ya wiki zaidi ya 34 analazimika kumsugua mumewe mgongoni na kiunoni kila siku na kumkanda tumbo lake.

No comments: