Saturday, September 29, 2012

Nani asiyejua Kondom? Unajua zilianza lini na wapi?


Nani asiyejua kazi ya Kondom? Lakini unajua kifaa hicho ambacho siku hizo husambazwa bure kilianza lini na wapi?

Tarehe halisi haifahamiki lakini katika karne ya 15 yaani miaka mia 6 iliyopita kondom zilikuwepo na zilikuwa zinatumika katika bara la Asia. Miaka mia sita iliyopita Kondom nchini china zilikuwa zinatengenezwa kutumia utumbo au mbuzi au kondoo. Na Matajiri walikuwa wakitumia Kondom zilizotengenezwa kwa karatasi ya hariri iliyopakwa mafuta.

Nako nchini Japan Kondom zilikuwa zikitengenezwa kwa magamba ya kobe au pembe za wanyama . Na ama pembe ilikuwa ikivaliwa kama kondom..ni huko Japan, miaka mia 6 iliyopita.
Ni katika karne iliyopita , mwaka 1900 kondom zilizotengenezwa kwa utumbo wa mbuzi na kondoo hata utumbo wa ngombe zilianza kuenea duniani. Enzi hizo zilikuwa zinatumiwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba isiyotakikana.

No comments: