Friday, July 6, 2012

Unamjua Mbuni? Kisayansi wanamuita Struthio camelus

Huyu ndio anaitwa Mbuni kwa Kiswahili ndio ndege mkubwa kuliko wote wanaoishi wanaopatikana Duniani kwa sasa. Kisayansi anaitwa  "Struthio camelus"  Jina hili limetokana na maneno ya Kilatin ambayo kwa Tafsiri  "Struthio" ni Mbuni na "camelus" ni ngamia. Yupo kwenye kundi la ndege wasioruka. Utafiti umeonyesha anapatikana katika nchi hamsini duniani. Wanaishi kwa kula mimea na Wadudu. Na urefu kati ya futi sita na Tisa, uzito  wa kati ya 90kg mpaka 130kg na uwezo wa kukimbia mpaka kufikia 100km/hr. Majike wana rangi ya kahawia na madume wana rangi nyeusi kwa sehemu kubwa ya miili yao.

Una ufahamu juu ya ndege huyu Mbuni? na wewe ongezea ya kwako hapa.

No comments: