Tuesday, July 26, 2011

WAHEHE HASIRA IMEPITILIZA. NI BALAA

Kutoka iringa-Tanzania.
Baba mmoja wa kihehe akiwa na mwanawe wakitoka machungani walikuwa wanajaribu kuwavusha ng'ombe wawili (mama ng'ombe na ndama) kukatisha mto.Kila yule mzee alipojaribu kumvusha yule mama ng'ombe,aligoma.Yule baba alihangaika sana bila mafanikio.

Mwishowe mtoto wa huyu baba wa kihehe akampa wazo babake kwamba watangulie kumvusha ndama then mama ng'ombe atafuata mwenyewe. Baba mtu kwa kinyongo alijaribu mbinu hiyo na ikafanikiwa kwa urahisi saana. Baba mtu alimwambia mwanawe atangulie na ng'ombe nyumbani, yeye atakuja baadaye. 

Yule baba hakuonekana nyumbani mpaka kesho yake walipomkuta ananing'inia mtini i.e kajinyonga. Mfukoni alikuwa na karatasi imeandikwa, 'SIWEZI KUVUMILIA, MWANANGU KANIZIDI AKILI'

Wahehe punguzeni hasira!

No comments: