
Serikali ya Mauritania imewakabidhi maafisa wa utawala wa Libya
aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini humo, Abdullah al-Senussi
Libya inataka
kumfungulia mashtaka bwana Senussi kwa makosa aliyoyafanya chini ya utawala wa
hayati Muamar Gaddafi. Mapema mwezi huu rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel
Aziz alisema kuwa bwana Sanusi aliyekuwa amekimbilia nchini humo, sharti kwanza
akabiliwe na sheria kwa makosa ya kuingia Mauritania kinyume na sheria. Senussi
alitoroka Libya baada ya mapinduzi ya mwaka jana ambayo yalimng'oa mamlakani
Muammar Gaddafi.
Pia anatakiwa na
Ufaransa pamoja na mahakama ya kimataifa kuhusu haki za bianadamu ICC kwa
makosa ya kukiuka haki za binadamu.
Ripoti za kukabidhiwa
kwake kwa watawala wa Libya, zilitolewa na televisheni ya taifa pamoja na
shirika rasmi la habari la Mauritania. Kulingana na ripoti, bwana Senussi
alikabidhiwa kwa wajumbe wa Libya walioongozwa na waziri wa sheria na haki wa
nchi hiyo. Lakini hadi sasa bwana Senussi hajulikani aliko.
No comments:
Post a Comment