Wednesday, June 8, 2011

Fikiria kama ni wewe ITAKUWAJE?

Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. 
Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao 
nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini 
kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga
wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula. Basi wakaamua 
wapike uyoga kidogo, na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika 
wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa 
hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala. 
Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani 
akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa 
wao amekufa.

Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha 
yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao 
wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele 
yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote.

 
Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. 
Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito 
wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake 
wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana 
mama yake.

Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nami nitubu
Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na Shamba 
boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani. 


Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani 
na kukuta wakigombana. Akawauliza,Baba na mama mnagombania 
nini humu ndani, badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa 
kugongwa na gari kule nje?


Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki 
wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

Fikiria kama ni wewe ITAKUWAJE?



No comments: