Friday, August 24, 2012

Adhabu ya doezi la wake za watu hii hapa...


Jamaa mmoja alikuwa na mke wake waliyependa sana. Kutokana na upendo huo jamaa alihakikisha mkewe anapata kila kitu anachotaka. Hata hivyo kwa bahati mbaya mwana mama huyo hakuwa muaminifu kama mume wake alivyotarajia kwani alikuwa na mpenzi mwingine (kibustani) ambae alikuwa akimuhudumia kila mumewe anapokuwa kazini. Mbaya zaidi ni kwamba dada huyo alikuwa akimlisha bwana huyo na kumnunulia nguo kwa fedha anazopewa na mumewe. Baada ya masiku kadhaa mumewe akapata hisia kwamba mkewe ana mtu mwingine kwani tabia zake zilianza kubadilika. Hata hivyo hakufanya papala.

Mwanamke aliporudi bila kujua kilichotokea, akachukua msosi na kukimbilia kwa doezi. Kwa bahati nzuri siku hiyo doezi huyo alikuwa amemualika rafiki yake mpenzi ili wafaidi pilau hivyo chakula lilipowekwa mezani tu jamaa wakaanza kukishambulia huku mke wa watu akiwamenyea nanasi ili washushie baada ya chakula. Ni baada ya kula robo ya chakula ndipo jamaa walipoanza kusikia harufu isiyo ya kawaida...hata hivyo wakaendelea kula huku kila mmoja alimuhisi mwenzie katoa hewa chafu. Dakika mbili baadae ndipo walipokutana na scud... Varangati lililozuka humo ndani halielezeki.

Mwenye mke aliporudi nyumbani akamkuta akiwa amevunjika mkono na uso umejaa manundu. alipomuuliza kulikoni mke akadai kapigwa na vibaka. Jamaa akaenda kuangalia uvunguni mwa kitanda na kukuta sahani ya pilau haipo...kumuuliza mkewe iko wapi? mama akabaki akipepesa macho. TALAKA ikafuatia....

No comments: