Friday, August 24, 2012

Toba kitandani..


Mwanaume mmoja alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa amepoteza fahamu kwa siku mbili. Alipozinduka akamuona mkewe akiwa pembeni ya kitanda akimuombea. Jamaa kwa upendo akamuita mkewe na kumwambia "Honey kabla sijafa kuna jambo inabidi nikwambie ili niweze kwenda mbinguni nikiwa safi" jamaa alimueleza mkewe taratibu. " Nimecheat...kwa muda mrefu nilikuwa nikifanya mapenzi na rafiki yako Samia, pamoja na mama Kay, yule jirani wetu wa nyumba ya tatu. Na hata yule house girl wetu aliyeondoka kwenda kwao nilisha wahi kulala nae wakati ulipoenda mkutano wa kikazi Arusha...Naomba unisamehe mke wangu nife vizuri" Jamaa alimaliza huku machozi yakimtoka. Kwa upendo mkewe akamshika mkono na kumwambia " Usijali honey, nimesha kusamehe, ila na mimi pia naomba unisamehe kwa kukuwekea sumu..."

No comments: