Tuesday, August 14, 2012

Dk Ulimboka awekwa mafichoni - YABAINIKA HAYUPO NYUMBANI, TAARIFA ZAKE ZAFANYWA SIRI, BABA, NDUGU, MARAFIKI WAGOMA KUZUNGUMZA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, 
Dk Stephen Ulimboka baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.
Picha na Fidelis Felix

WINGU limegubika sakata la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka siku moja baada ya kurejea nchini, huku watu wake wa karibu akiwamo baba mzazi, wakigoma kusema chochote kumhusu.


Dk Ulimboka alirejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kwa takriban mwezi mmoja na nusu, baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

Ingawa wakati wa ugonjwa wake baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakitoa maelezo mbalimbali, jana wote waligoma kusema chochote, huku jitihada za gazeti hili kumpata nyumbani kwake zikigonga mwamba.



Baba mzazi wa Dk Ulimboka, Stephen Mwaitenda aliweka wazi kuwa ni vigumu kumwona daktari huyo jana.Takriban watu wote waliofika nyumbani kwa Mzee Mwaitenda jana kumjulia hali Dk Ulimboka waliambiwa kuwa hayupo nyumbani.



Mwaitenda alilieleza gazeti hili kuwa ana furaha kuwa mtoto wake alirejea nchini salama licha ya kupelekwa Afrika Kusini akiwa taabani kutokana na kipigo. Alipotakiwa kueleza juu ya kile kilichompata, mtoto wake huyo alisema: "Mungu na Steven mwenyewe (Dk Ulimboka) ndio wanaojua kilichotokea."

Aliongeza: “Kweli nimefurahi kwamba mwanangu amerudi, lakini siwezi kuelezea nini kilimtokea alipotekwa," alisema Mwaitenda.

Alisema Dk Ulimboka hayupo nyumbani na hajui kwamba angerudi wakati gani. "Hata kama angekuwapo, ni vigumu kumwona," alisema.


HABARI ZAIDI GONGA KWENYE CHANZO CHA HABARI HII HAPA CHINI:-

http://www.mwananchi.co.tz/ulimboka awekwa mafichoni.


No comments: