Monday, August 27, 2012

Huyu ni Mwanafunzi Makini anitwa Dayness


Mwalimu wa somo la hesabu alimuuliza mwanafunzi wake "Dayness, kama kuna ndege mia kwenye mti, ukichukua bunduki yako na kuwapiga ndege ishirini na saba, ndege wangapi watabaki kwenye mti? Dayness akamjibu "Hakuna ndege atakaebaki, wote wataruka na kukimbia kwa kuogopa kishindo cha bunduki" Mwalimu akamwambia " Hapana, watabaki ndege sabini na tatu. Hata hivyo nimependa jinsi unavyofikiri mbali zaidi...uko makini.

Dayness akamwambia  "Mwalimu na mimi nina swali, kama kuna wanawake watatu kwenye mgahawa wanakula 'cone icecream' mmoja anakula kwa kuilamba, mwingine anakula kwa kuimega vipande na wa tatu anakula kwa kuinyonya, unadhani ni yupi aliyeolewa (mwenye mume) kati ya hao? Mwalimu akamjibu "Bila shaka ni yule anaekula kwa kuinyonya"  Dayness akamwambia "hapana mwalimu umekosea...ni yule  mwenye pete ya ndoa, hata hivyo na mimi  nimependa sana jinsi unavyofikiri mbali zaidi..."

No comments: