Monday, August 27, 2012

Uingereza haitaingia tena kwa nguvu ubalozi wa Ecuador


Rais wa Ecuador, Rafael Correa, anasema kuwa Uingereza imeacha kile alichosema ni tishio la kuingia kwenye ubalozi wa Ecuador mjini London kumkamata muasisi wa Wikileaks, Julian Assange.
Rais wa Ecuador, Rafael Correa

Bwana Correa alisema kuwa sasa anaona ugomvi wa kidiplomasia baina ya nchi mbili hizo umekwisha.Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza ilipeleka barua kwa ubalozi huo iliyokusudiwa kuruhusu mazungumzo kuhusu Bwana Assange kuanza tena, lakini Uingereza imekanusha kuwa ilitishia wakati wowote kuingia ubalozini.

Bwana Assange anatakiwa aende Sweden, ambako wakuu wanamsaka kutokana na tuhuma za ubakaji.
Amepata hifadhi ya kisiasa nchini Ecuador, lakini anaweza kukamatwa akitoka kwenye ubalozi wa Ecuador mjini Londo

No comments: