![]() |
Tsvangirai na mpenzi wake |
.
Mahakama nchini Zimbabwe imesitisha harusi ya Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai iliyotarajiwa kufanyika leo Jumamosi kama ilivyokuwa imepangwa. Mahakama imesema kuwa Tsvangirai tayari ana mke
Mapema wiki hii
mahakama kuu nchini humo ilitupilia mbali madai ya Locadia Tembo aliyesema kuwa
yeye ni mke wa kitamaduni wa Bwana Tsvangirai na kusema kuwa ndoa za kitamaduni
hazitambuliki kisheria. Lakini sasa Hakimu amekubaliana na Locadia na kuamuru
harusi iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi haitafanyika tena. Hii ni licha
ya baadhi ya viongozi wa nchi mbali mbali walioalikwa kwenye harusi kuwasili
nchini humo. Mawakili wa Tsvangirai wanataka mahakama kutoa amri ya dharura na
kuruhusu harusi hiyo kuendelea kama ilivyopangwa.
Kesi nyingine ambayo
mahakama ilisikiza leo dhidi ya Tsvangirai ni ya mwanamke mmoja kwa jina
Nozipho Shilubane aliyesema kuwa Waziri Mkuu huyo aliahidi kumuoa. Baadhi ya
wadadisi wanasema kuwa kesi hiyo ni dalili ya njama za kisiasa kumpaka matope
waziri mkuu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao. Tsvangirai
atatoana jasho na rais Robert Mugabe katika uchaguzi huo. Lakini wengine
wanasema kuwa Tsvangirai hana wa kulaumu ila yeye mwenyewe kwani amejihusisha
na wanawake wengi baada ya mke wake kufariki katika ajali ya barabarani mwaka
2009 baada ya waziri mkuu kuchukua wadhifa wake.
Mwandishi wa BBC Brian
Hungwe aliyepo mjini, Harare, anasema kuwa harusi hiyo ilipangwa kufanyika
katika mtaa mmoja wa kifahari mjini Harare. Rais Mugabe anatarajiwa kuandaa
dhifa maalum kwa viongozi wa nchi za kiafrika walioalikwa kuhudhuria.
Source: BBCswahili
No comments:
Post a Comment