Tuesday, September 25, 2012

Iran yabana huduma za Google


    Serikali ya Iran imebana huduma za mtandao wa tafuta tafuta wa Google,pamoja na huduma 
    Serikali ya Iran imebana huduma za mtandao wa tafuta tafuta wa Google, pamoja na huduma zake za barua pepe za Gmail. Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kama tahadhari kufuatia maandamano makubwa ambayo yalikumba nchi za Kiislamu zilizokerwa na filamu ya Marekani iliyomkejeli Mtume Muhammad na dini ya Kiislamu.

    Filamu hiyo ilipeperushwa kupitia mtando wa kijamii wa YouTube ambao unamilikiwa na Google. Baadhi ya wanablogu, wamekemea hatua hiyo ya serikali kama inayolenga kukandamiza uhuru wa kujieleza Maafisa wa utawala wamekuwa wakijiandaa kuzindua mtandao mwingine wa internet utakaotumika tu nchini humo ili wananchi wakome kutumia mitandao ya kigeni. Kwa mujibu wa maafisa wakuu, hatua hiyo italinda mtandao wa internet wa Iran kutokana na uvamizi kutoka nje.

    SOURCE: BBC Swahili

No comments: