![]() |
Kanisa katoliki nchini Ujerumani |
Sheria kali itakayowashurutisha waumini wa kikatoliki kulipa kodi ya
kanisa la sivyo wanyimwe sakramento imepitishwa nchini Ujerumani. Maaskofu waliopitisha sheria hiyo wamesema
kuwa yeyote atakayekosa kulipia kodi ya kanisa ambayo ni asilimia nane ya
mapato yao watanyimwa sakramento na kisha kutotambuliwa kama wakatoliki. Maaskofu hao wameshtushwa na idadi ya
watu wanaoendelea kuasi ukatoliki. Wanasema
kuwa hatua kama hii ya kuasi dini itakuwa ni kwenda kinyume kabisa na maadili
ya jamii.
Watu wote
waliosajiliwa rasmi kama wakatoliki, waprotestandi au wayahudi, hulipa asilimia
8 hadi 9 ya mapato yao ya kila mwaka. Kodi hiyo ilianza kutozwa karne ya 19
kama fidia ya kutaifishwa kwa mali ya kanisa nchini humo. Idadi ya wakatoliki
nchini Ujerumani ni asilimia 30, lakini idadi ya watu nchini Ujerumani wanaoasi
kanisa hilo iliongezeka hadi watu 181,000 mnamo mwaka 2010, huku lawama
zikitolewa kwa kashfa nyingi za ngono zilizolikumba kanisa hilo wakati huo.
Maaskofu hao
wamechukua hatua baada ya kushtushwa na ongezeko la waumini wa kanisa hilo
wanaoasi dini, pamoja na profesa mmoja aliyestaafu Hartmut Zapp kutangaza mwaka
2007 kuwa kamwe hatalipa kodi hiyo ingawa atasalia kuwa muumini wa kikatoliki. Iliarifiwa
kuwa profesa huyo alitaka kuendelea kupokea sakramento na kuendelea kutambulika
kama mkatoliki ingawa maaskofui walipinga hilo na sasa kesi kati ya profesa
huyo na kanisa itafikishwa mahakamani siku ya Jumatano.
Source: bbcswahili.com
Source: bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment