Saturday, September 29, 2012

Je wajua kuwa mtu na mkewe wakiishi kwa zaidi ya miaka 25 huishia kufanana?


Mwalimu Nyerere
Si hadithi bali ni kweli kwamba , mtu na mkewe wakiishi kwa zaidi ya miaka 25 huishia kufanana! ukitaka kuthibitisha hilo hebu muwaangalie bibi na babu, ukiwa wewe ni mtu mzima hebu waangalie wazazi wako wote wawili?
Hebu tazama picha ya Hayati baba wa Taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Mama Maria? Unaonaje?
Mama Maria Nyerere
Lakini kitu gani kinasababisha hali hii ya mtu na mkewe kufanana baada ya kukaa pamoja kwa miaka 25 au zaidi? Wataalamu wanasema, ikiwa kuna upendo kati yenu, hii itachangia? kwa vile kwa miaka 25 mume na mke hucheka pamoja, kulia pamoja, wakati wa msiba uhuzunika pamoja, wakati wa matatizo na mihangaiko wanakabiliana nayo pamoja hivi vinasaidia kugeuza shepu na sura au uso wa mtu hivyo mume na mkewe huishia kufanana. vyakula pia vinasaidia kuwafanya wafanane. kwa vile wanakaa pamoja kwa miaka mingi, mume na mkewe hula vyakula vya aina moja na kukaa mazingira ya aina moja inasaidia kuwafanya wafanane.
Ni utafiti uliofanywa na Dr. Zajonc(ZI-onz) akishirikiana na Pamela Adelmann, Sheila Murphy na Paula Niedenthal na kuchapishwa katika jarida la kisayansi la , Motivation and Emotion.
Je unataka kujua utakapozeeka utafanana vipi? Kazi rahisi sana. Wataalamu wakiongozwa na Dr. Zajonc(ZI-onz) wanasema kama wewe ni mwanamume hebu muangalie baba mkwe wako, na kama wewe ni mwanamke, muangalie kwa umakini mama mkwe. Urefu unaweza kuwa tofauti lakini sura, utakapozeeka utafanana kama wakwe zako.

No comments: