Thursday, September 13, 2012

Madaktari nchini Kenya leo waanza mgomo


Madaktari nchini Kenya leo wanaanza mgomo wao kushinikiza nyongeza ya mishahara huku sekta ya afya ikiwa katika tisho la kuathirika. Wanajiunga na Walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiendelea na migomo kwa wiki ya pili sasa.
Madaktari hao kutoka hospitali za umma wanasema kuwa serikali imepuuza onyo lao la kugoma ikiwa haitatimiza matakwa yao. Wanasema kuwa serikali iliwahadaa baada ya kukataa kutekeleza makubaliano waliyoafikia mwezi Disemba mwaka jana ya kutimiza matakwa yao ya mishahara bora na mazingira mazuri ya kazi na mafunzo ya kitaaluma.

No comments: