![]() |
Bendera ya Marekani ikiwa chini baada ya jengo la ubalozi kuharibiwa |
Maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la. Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa.
Wameelezea mashambulio
hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi
ya jihad huenda yalihusika. Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na
uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed. Takriban
waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo
Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
![]() |
Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens |
Awali waandamanaji
walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya
kutoa machozi kuwa tawanya. Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichoma
moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali
ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
No comments:
Post a Comment