Thursday, March 3, 2011

TUWE WAANGALIFU TUNAPOTAKA KUDANGANYA, SOMA HII

Jamaa ana mpenziwe wamependana kiukweli, wanavodai wao nakuelezana hivyo kiasi kwamba password za bank card, e-mail nk. wamepeana.Wameahidiana hawatakuja kusalitiana milele. 

Wote hawa wana ujuzi kutumia mitandao ya kijamii kama huu.Wote wapo kwenye mtandao fulani na siku ya siku wakajikuta wanachati kwenye thread na mara Ku PM each other wakitumia majina yao ya bandia.Na kila mmoja asijue anachat na nani hasa.Ikafika point wakakubaliana kuwa wapenzi kwani walikua wanaambiana hawana wapenzi wengine.

Mambo yakaendelea hivi kule home wakirudi kila mtu akijifanya mtakatifu kwa mwenzie na kuonyeshana mapenzi motomoto wala hathubutu kutaja mchumba mpya wa kwenye mtandao. 

Basi huko mtandaoni wakati wakichat wakakubaliana kwamba imefika muda sasa wakutane na kufahamiana zaidi. Mwanaume kampa location mwanamke kwamba akae hapo taxi itakuja kumchukua na kumpeleka hotel na chumba alipo.Siku haikukawia ikafika dada kachukuliwa kama ilivyo pangwa kupelekwa huko kwa mpenzi mpya wa mtandaoni. Gari imefika Hotelini dada kapelekwa kaonyeshwa chumba, kagonga mlango, mlango ukafunguliwa......................guess what happened!!!!!alafu uniambie hii kesi itapelekwa mahakama gani?
 

No comments: