Sunday, August 19, 2012

Awamu ya JK yaongoza kuficha fedha nje ya nchi

YAFUATIA YA NYERER, MKAPA NA YA MWINYI YASHIKA MKIA


Rais Jakaya Kikwete
RIPOTI ya utafiti wa utoroshaji wa fedha nchini kwenda kufichwa katika benki za nchi za nje ikiwamo Uswisi uliofanywa na na  Shirika la Global Financial Integrity umeonyesha kuwa fedha nyingi kutoka Tanzania zilitoroshwa kati kipindi cha utawala wa awamu ya nne kati 2005 na 2009.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuhusu utoroshwaji wa fedha kwa njia haramu kutoka Afrika kwenda mataifa yaliyoendelea, ambayo gazeti hili limeipata, katika  kipindi hicho fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).  

Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa katika kipindi cha utawala wa kwanza ulioishia 1985, fedha zilizofichwa nje zilikuwa Dola 3,493.3 milioni (Sh5.5 trilioni) na katika awamu ya tatu  kati ya 1995 hadi 2005, zilikuwa Dola 2,108.8 milioni (Sh3.3 trilioni) wakati katika awamu ya pili zilitoroshwa Dola 529.1 milioni (Sh846 bilioni).

Utafiti huo wa Shirika Global Financial Integrity unaonyesha pia nchi 20 za Afrika zinaongoza kwa kuficha fedha nje ya nchi, Nigeria ikiongoza.

Jumla ya Dola za Marekani 1.8 trilioni zimefichwa katika benki mbalimbali nje ya nchi kutoka katika nchi za Kiafrika katika kipindi cha mwaka 1970 hadi 2009.

KUSOMA ZAIDI HABARI HII GONGA LINK YA MWANANCHI HAPO CHINI" 

No comments: