
Mji huo mpya kwa ajili ya wanawake pekee ukiwa na viwanda mbalimbali unajengwa nchini Saudi Arabia ambapo katika mji mzima wanawake wataishi wenyewe na wakifanya kazi bila ya kuwepo ya hata mwanaume mmoja.
Katika kuwapa nafasi wanawake kufanya kazi kwa uhuru kama wanawake wa sehemu zingine duniani, Saudi Arabia inatarajia kujenga mji wa kisasa kwaajili ya wanawake pekee. Mji huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 133 utaanza kujengwa mwanzoni mwa mwakani karibu na mji wa mashariki mwa Saudi Arabia wa Hafuf. Mji huo utakuwa na viwanda vya nguo, madawa na vyakula na inakadiriwa kuwa jumla ya wanawake 5,000 watapata ajira.
Hatua hii ya kuanzishwa kwa mji wa wanawake pekee inakuja ili kuwapa nafasi wanawake wa nchi hiyo, inayofuata sheria kali za Kiislamu, kuendana na wakati na kufanya kazi na pia kuwapa mazingira ya kazi yatakayoenda sambamba na sharia za kiislamu.
Mamlaka ya viwanda ya Saudia, Modon imesema kuwa ina mpango mwingine tena wa kuanzisha mji wa pili wa wanawake pekee mbali na mji wa Hafuf.
No comments:
Post a Comment