mlima Kilimanjaro |
Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kuvipigia kura vivutio vya kitalii vya Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti, ili vipate kuingia kwenye shindano la maajabu saba ya Asili katika bara la Afrika.
![]() |
Ngorongoro crater |
Zoezi hilo linaendeshwa kwa kupiga kura kupitia tovuti ya http://sevennaturalwonders.org. ambalo linashindanisha vivutio vya utalii 12, katika Bara la Afrika, ambapo Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vingi katika orodha hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, ilisema shindano hilo jipya linashindanisha vivutio mbalimbali vya asili vya vinavyopatikana katika kila bara.
No comments:
Post a Comment