ha

Mwili wa Zenawi ukiwasili Adis Ababa
Mwili wa aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Melez Zenawi, uliwasili jana usiku katika mji mkuu wa
nchi hiyo Adis Ababa na kwa sasa umehifadhiwa katika Ikulu hadi mazishi yake
yatakapofanyika.
Maelfu ya raia wa nchi hiyo walimiminika katika barabara za mji
huo jana jioni wakati mwili wake ulipowasili kutoka mji mkuu wa Ubelgiji,
Brussels. Meles, ambaye alikuwa na umri wa miaka 57, aliaga dunia ghafla
kutokana na maambukizi wakati alipokuwa akitibiwa.
Kifo
cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombea madaraka hali ambayo ingeweza
kuathiri amani ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, naibu waziri mkuu
Hailemariam Desalegn ataliongoza taifa hilo hadi mwaka 2015 wakati uchaguzi
mkuu utakapofanyika.
Utawala
wa Bwana Zenawi ulishutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuna hofu kuwa Waziri
Mkuu mpya huenda asiwe na uzoevu wa kushughulikia na kutatua uhasama wa kisiasa
unaoendelea nchini humo. Zenawi amesifika kwa kuiongoza Ethiopia kufikia
mafanikio makubwa ya maendeleo na uchumi, lakini wakosoaji wake wanasema licha
ya hayo yote utawala wake haukuruhusu uhuru wa siasa za vyama vingi na kuwa
viwango vya ukiukwaji wa haki za binadamu bado viko juu.
Bwana
Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na
nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998. Meles Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991
baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment