Tuesday, August 14, 2012

Wawili wafa huku kumi na nne wakiokolewa katika mkasa wa ndege za Uganda


Ajali ya ndege ya kijeshi ya Uganda


Maafisa kumi na wanne wa  kiufundi wa Uganda waliokuwa katika ndege mbili za kivita iliyopotelea katika angaa la Kenya zikienda Somalia wameokolewa wakiwa hai.

Afisa wa uokoaji kutoka katika shirika la wanyapori nchini Kenya amesema kuwa watu hao waliokolewa kutokana na ndege zao kutoshika moto baada ya kuanguka huku wakipata maiti ya wanajeshi wawili kutoka kwenye ndege nyingine iliyoanguka na kushika moto.

Awali,msemaji wa jeshi la Kenya Bogita Ongeri alisema ndege mbili zilikuwa zimepatikana zikiwa zimeungua ila watu waliokuwemo ndani wanaokadiriwa kuwa kumi  hatima yao ilikuwa bado haijafahamika.

Ndege zingine mbili ambazo pia zilianguka katika mlima huo zilipatikana jana na watu saba walikuwa katika ndege hiyo waliokolewa wakiwa hai.

Ndege hizo za kivita zilizonunuliwa nchini Urusi zilikuwa zinakwenda Somalia katika eneo la Kismayo kupambana na wanamgambo wa Al-Shabab mwezi huu wa nane. AMISOM imekuwa ina wanajeshi elfu 17 wakiwemo kutoka Uganda ambao wanakabiliana na kundi la Al-Shabab.

Habari hii ni kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali


No comments: