
Balozi wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi. Balozi huyo alisemekana kuwa miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.
Idara ya mambo ya
ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisa mmoja wa ubalozi huo
ingawa bado haijataja jina lake. Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia
yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani. Wakati huohuo, waziri wa
mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.
Serikali ya Libya
imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga. Ubalozi huo uliteketezwa na watu
waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini
Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed. Wanamgambo hao
wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali
walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya
kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya
Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya
ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu
Mtume Mohammed. Kwa wakati mmoja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi
huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.
No comments:
Post a Comment