Monday, September 10, 2012

Soma mpaka mwisho tafadhari...


"Mimi na girlfriend wangu tulikuwa tunapendana sana. Tulikuwa tumeishakuwa pamoja kwa muda wa miaka minne hivi, na hivyo tukawa tumeamua kuoana. Kulikuwa na jambo moja dogo tu lililokuwa likinisumbua sana; mdogo wake wa kike ambae alikuwa mzuri sana.

Huyo binti (shemeji yangu) alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja hivi, muda wote alipendelea kuvaa sketi fupi sana na fulana nyepesi au brauzi zinazoonesha mwili wake na jinsi kifua chake kilivyo alikuwa hahitaji kuvaa sidiria. Pamoja na binti huyu kuwa mwembamba kiasi, alikuwa na umbo la ajabu. Kiuno chake kiliumbwa mithiri ya nyigu weusi....

Tatizo ni kwamba mara nyingi binti alipokuwa akiniona alikuwa na tabia 
ya kujipitisha pitisha na kuinama mbele yangu ili kunionesha mtaji wake. 
Kusema kweli nilikuwa navutiwa sana na uzuri wake, lakini nilikuwa namuheshimu 
sana mchumba wangu. Na pia nilijua alikuwa ananifanyia makusudi maana 
alikuwa hafanyi hivyo kukiwa na watu wengine...bila shaka alikuwa ananitaka. 
Siku moja binti huyo alinipigia simu niende nyumbani kwake nikaangalie kadi za 
mialiko ya arusi alizokuwa amechapisha. Nilipofika (wakati naingia ndani) 
akaninong'oneza kuwa ananitamani sana na kamwe hawezi kujizuia. Akaendelea 
kunieleza kuwa anahitaji tufanye mapenzi kabla sijafunga ndoa na dada yake 
ili nisijisikie vibaya kwamba natoka nje ya ndoa....

Nilipigwa na bumbuazi na hasa kutokana na nguo za nusu uchi alizokuwa 
amevaa. Kabla sijamwambia lolote akaniwahi "Mi natangulia juu (ghorofani) 
kwenye chumba changu, kama unahitaji nikupe kitu kitamu njoo haraka 
kabla mashetani yangu hayajapoa..." akageuka na kukimbilia chumbani kwake.

Haraka nikageuka na kuelekea mlango mkubwa wa kutoka nje. Nikafungua na 
kutoka kuelekea kwenye gari yangu. Loh! kwa mshangao mkubwa nikaona
pale nje familia yote imekusanyika na waliponiona nikitoka wakanipigia 
makofi na vigelegele kwa furaha.

Huku machozi yakimtoka kwa furaha, baba mkwe akaniambia "Tumefurahi 
sana kwamba umeshinda mtihani mdogo wa uaminifu ulioandaliwa na familia. 
Tuna hakika wewe ndie mwanaume pekee unaefaa kumuoa binti yetu...karibu 
katika familia....

Kitu cha maana nilichojifunza siku hiyo, ni umuhimu wa kuweka condom 
ndani ya gari badala ya kutembea nazo mfukoni.....  

No comments: