Zaidi ya watu mia mbili arobaini wamefariki dunia katika mkasa mkubwa wa
moto uliotokea katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mji mkubwa zaidi
nchini Pakistan, Karachi. Mamia kadhaa ya watu waliruka kutoka paa la jengo hilo
wakijaribu kujiokoa lakini wengi wakiwemo wanawake na watoto walinaswa katika
jengo hilo lenye ghorofa nyingi.
Karibu magari arobaini
ya wazima moto yalipambana na moto huo usiku kucha. Walioshuhudia moto huo
mkubwa, walielezea kuona watu wakining'inia katika madirisha ya ghorofa za juu
na kisha kuruka chini wakijaribu kujiokoa. Afisa mmoja mkuu nchini humo alisema
kuwa madirisha yalikuwa yamefungwa kwa vyuma na kiwanda hicho hakikuwa na
vyumba salama vya kutorokea wakati moto ukizuka.
No comments:
Post a Comment