Thursday, October 11, 2012

Papa ahubiri kwa Lugha ya Kiarabu

Papa Benedict wa kumi na sita
(Picha Kutoka maktaba)
Papa Benedict wa kumi na sita, ametoa baraka zake kwa lugha ya kiarabu katika hotuba yake ya kila wiki kwa dunia nzima. Hotuba hiyo hupeperushwa moja kwa moja kupitia televisheini. Papa alisema kuwa anawaombea watu wote wanaotumia lugha ya Kiarabu.
Kabla ya maombi yake, padri mmoja pia alisoma hotuba ya wiki kwa mara ya kwanza katika lugha ya Kiarabu. Maafisa katika makao makuu Vatican walisema kuwa hatua hiyo huenda itawafarijji wakristo Mashariki ya kati, wengi wao ambao wamekuwa wakiondoka kutoka eneo hilo wakisema kuwa wanahofia usalama wao.

No comments: