Wednesday, August 22, 2012

Breaking news - Mkuu wa Wilaya ya Serengeti afariki dunia


MKUU wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Kapteni mstaafu James Yamungu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa amelithibitisha kuhusu kifo cha Kapteni Yamungu kilichotokea saa 5 asubuhi katika hopitali  ya Muhimbili ambako alifikishwa hapo Agosti 21, mwaka huu  akitokea Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza alikokuwa amelazwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti,  Magohe Zonzo ambaye alikuwa akimuuguza Bugando aliliambia gazeti hili kuwa taratibu za mazishi zinaandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Agosti 16, mwaka huu Yamungu alifikishwa katika Hospitali Teule ya Nyerere DDH wilayani Serengeti na kulazwa kwa saa tatu kisha kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando.

Kabla ya kufikishwa hospitalini hapo inasemekana mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Anita Motel iliyoko mjini Mugumu ambako alikuwa anaishi kufuatia nyumba ya Mkuu wa Wilaya kuwa inafanyiwa ukarabati alibaini Yamungu kuwa amezidiwa hivyo alitoa taarifa.

Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ililazimika kufungua mlango na kumkuta hajitambui  na kumpeleka hospitali ya Nyerere kabla ya kumhamishia Bugando.

Yamungu amehamia wilayani Serengeti mwaka huu akitokea Wilaya ya Meatu kufuatia mabadiliko ya wakuu wa wilaya.

No comments: