
Watu wanne wamekufa na
wengine wanane kujeruhiwa baada ya ndege moja kuangukaa jana katika mbuga ya
taifa ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya, moja ya mbuga iliyo kivutio
kikubwa cha watalii, Afrika Mashariki.
Afisa kutoka Mamlaka
ya Anga nchini Kenya, Mutia Mwandikwa amethibitisha kuanguka kwa ndege hiyo.
Mutinda amesema
miongoni mwa waliokufa ni pamoja na watalii wawili kutoka Marekani na marubani
wawili wa ndege hiyo, ambao ni raia wa Kenya.
Kwa mujibu wa idara ya
polisi ndege hiyo iliyokuwa imebeba watalii ilianguka muda mfupi baada ya kupaa
kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Ngerende ulioko katika mbuga hiyo ya wanyama ya
Maasai Mara. Miongoni mwa
waliojeruhiwa ni pamoja na raia wanne wa Marekani, wawili kutoka Jamuhuri
ya Czech na wawili kutoka Ujerumani.
Majeruhi hao
walisafirishwa kwa ndege nyingine hadi Nairobi ambako wanaendelea kupata
matibabu.
No comments:
Post a Comment