Tuesday, September 11, 2012

Uongo hauna dini...na njia yake ni fupi. soma hapa

Mwalimu wa somo la maadili ya kikristo (Christian ethics) katika shule ya seminari, aliwaambia wanafunzi wake, kesho tutazungumza kuhusu 'watu waongo'  hivyo kwa kujiandaa na somo hilo, kila mwanafunzi akasome injili ya Marko sura ya kumi na saba (Marko 17).

Kesho yake mwalimu akaingia darasani na kutangaza "wale waliosoma injili ya Marko sura ya 17 wapite mbele". Bila kuchelewa robo tatu ya darasa wakainuka katika viti na kwenda mbele ya darasa. Mwalimu huyo akatangaza tena "Nyie mliobaki kwenye viti mnaweza kubeba vitabu vyenu na kwenda nje maana hawa ndio waongo ninaotaka kuzungumza nao"

Injili ya Marko ina sura 16 tu...

No comments: