Thursday, October 11, 2012

FUKWE ZAFUNGWA AFRIKA KUSINI KUFUATIA KUVAMIWA NA PAPA WEUPE WALIOKUWA WANAFUATA MZOGA WA NYANGUMI.

Sehemu kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza kushambuliwa na jamii ya papa weupe. Inasemekana kiumbe mkubwa kuliko wote anayeshi duniani kwa sasa ni nyangumi

Wafanyakazi wa mamlaka ya Usalama wa baharini nchini Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kusogeza mzoga wa Nyangumi nchi kavu kwa ajili ya kwenda kuuzika.

Mzoga wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.

Mamlaka husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari.
Mzoga wa Nyangumi ukipimwa urefu.
 Mashine aina ya bulldozer ikiutoa huo mzoga huo ufukweni mwa bahari.
Wataalamu wakiendelea kuchukua vipimo vya nyangumi huyo
Jitihada za kuutoa mzoga zikiendelea
Nyangumi akiwa tayari amepakizwa kwenye Lori aina ya "low loader".
Nyangumi huyo alisafirishwa kunakohusika.

No comments: