Tuesday, July 31, 2012

MTIKISIKO - WAALIMU WAGOMA KILA KONA YA TANZANIA


Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo.Picha na Elizabeth Edward
WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA 

Waandishi Wetu
NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na Waalimu wakuu na Wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na Waalimu katika ngazi ya usuluhishi. Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa Waalimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

KUSOMA ZAIDI GONGA HAPA:
  

No comments: